Tafsiri ya Kiswahili

Mradi wa Ushirikiano wa Kuhifadhi Habari kwenye Filamu wa Afrika, yaani “The Cooperative Africana Materials Project” (CAMP) ulianzishwa mwaka 1963. Mradi huu ni juhudi za pamoja baina ya maktaba za utafiti duniani na Kituo cha Maktaba za Utafiti (Center for Research Libraries, CRL). Madhumuni ya mradi huu ni kuendeleza hifadhi ya machapisho na nyaraka zinazohusika na kadri ya nchi hamsini za kusini mwa Jangwa la Sahara*; pia kuhakikisha watafiti wanapata haya machapisho.

* Mradi wa Ushirikiano wa Kuhifadhi Habari kwenye Filamu za Mashariki ya Kati, yaani “The Middle East Materials Project” (MEMP), unajumuisha nchi tano za Afrika ya Kaskazini, ikiwa ni pamoja na Misri, Libya, Tunisia, Algeria na Morocco, pamoja na machapisho ya lugha ya Kiarabu kutoka Sudan.

Nchi na Machapisho Yanayoshughulikiwa na CAMP

Mradi wa CAMP hupata jozi za microform zenye thamani kubwa na huruhusu kurudufu nakala halisi na pekee za machapisho ya utafiti toka Amerika Kaskazini, Ulaya na Afrika. Mradi huu hukusanya nakala za microform za machapisho haya kama ifuatavyo:

  • Magazeti yaliyochaguliwa, pamoja na yale yaliyoagizwa na kupokelewa wakati huo
  • Majarida 
  • Machapisho ya serikali
  • Nyaraka binafsi na za mashirika mbalimbali
  • Nyaraka binafsi za wanahistoria, waandishi wa habari, wana-anthropolojia, wanajiografia na viongozi wa serikali
  • Maandishi katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania, Kijerumani, lugha zingine za Ulaya, Kiswahili, Kixhosa, Kizulu na lugha zingine za Kiafrika.

Mradi wa CAMP hujumuisha machapisho mengi ya msingi yenye takwimu na habari za historia, siasa, isimu ya lugha, uchumi na jiografia, ambayo hayapatikani mahali pengine popote. Maktaba wanachama wanaweza kutegemea mkusanyiko huu mkubwa wa microform za magazeti na majarida, hivyo kukwepa gharama kubwa za kuagiza, kuorodhesha na kuhifadhi  machapisho haya kila mwanachama peke yake.

Machapisho ya Serikali katika CAMP

Mifano halisi ya machapisho husika kutoka sehemu mbalimbali ni machapisho ya serikali yahusuyo nchi za Kiafrika kabla ya uhuru, yaani Government Publications Relating to African Countries Prior to Independence (wachapishaji wake ni East Ardsley, U.K.: Microform Academic Publishers, chini ya Chama cha Masomo ya Kiafrika, yaani the African Studies Association cha Uingereza). Haya machapisho yanahusiana na nchi za Cameroon, Gambia, Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Machapisho mengine ya serikali za Afrika ni pamoja na magazeti rasmi na ripoti za benki. Pia kuna machapisho rasmi ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi wa Afrika, yaani the United Nations Economic Commission for Africa iliyopo Addis Ababa, Ethiopia. Machapisho mengine yanayohusiana na Afrika yanayotolewa na Shirika la Marekani la Maendeleo/Misaada ya Kimataifa, yaani the US Agency for International Development.     

Nigeria

Machapisho ya CAMP yanahusu mada mbalimbali kama vile vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Biafra, kilimo, ukoloni, uchumi na biashara, mawasiliano, mali asili na elimu. Machapisho mengine katika kundi hili ni yale yahusuyo historia ya ukoloni Lagos na miji mingine, pamoja na yanayohusu maamuzi ya kiutawala juu ya hali ya nchi. Mradi wa CAMP huhifadhi magazeti ishirini na tisa katika filamu za microform.

Sahel

Mradi wa CAMP ulinunua mkusanyiko wa nyaraka na tasnifu kutoka eneo la Sahel, yaani Sahel: Documents and Dissertations Collections (wachapishaji wake ni East Lansing, MI: Sahel Documentation Center, Michigan State University). Haya machapisho kwenye filamu za microfiche yana habari za kinaganaga na orodha ya machapisho kuhusu kilimo, hifadhi na mali asili, maendeleo, ukame na njaa, elimu, afya, mifugo, fasihi simulizi, wanawake, kazi, na usafiri. Nchi husika ni Mali, Niger, Burkina Faso, Chad, Mauritania, Senegal na Gambia. Mengi ya haya machapisho ni ya kipekee kwamba ni nyaraka za serikali ya Marekani na Afrika ambayo hayawezi kupatikana kwa njia nyingine.

Liberia, Cote d’Ivoire, Gambia, Togo

Mradi wa CAMP huifadhi Nyaraka za Albert Porte, yaani Albert Porte Papers, ambazo huhusisha mkusanyiko mkubwa wa magazeti ya Liberia yaliyotolewa katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini. Mkusanyiko mwingine, the Collection of the Honourable Louis Arthur Grimes, 1883-1945, hujumuisha nyaraka kuhusu ombi la Liberia kutaka msaada wa Umoja wa Mataifa mwaka 1931. Kuna machapisho mengi ya serikali kutoka au kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zote hizi nne.

Nchi Zinazozungumza Kireno Africa

Mradi wa CAMP ulinunua mkusanyiko wa magazeti sabini na moja ya lugha ya Kireno kutoka Angola, Cape Verde, Guinea-Bissau, Mozambique, Sao Tome and Principe, na Ureno.

Kusini mwa Afrika

Mradi wa CAMP umekusanya mkusanyiko muhimu wa filamu za microform za nyaraka, majarida, magazeti, na machapisho ya serikali katika ngazi za kitaifa, kimikoa na mijini. Hii ni pamoja na nyaraka za harakati za uhuru kama zile za African National Congress (ANC) ya Afrika Kusini na South West Africa People’s Organization (SWAPO) ya Namibia. Mradi wa CAMP ulipiga filamu ya the Carter-Karis Collection, 1920-1965 na baadaye ulichapisha toleo la fahirisi (index) yake uliofanywa na Susan G. Wynne kama South African Political Materials: A Catalogue of the Carter-Karis Collection (Bloomington, IN: South African Regional Archives Project, 1977). Hii imefanya haya machapisho ya harakati za siasa za watu weusi wa Afrika Kusini kuwa mojawapo ya nyaraka zinazotumiwa kwa wingi kati ya zile ambazo mradi wa CAMP ulishajipatia.

Huu mkusanyiko wa machapisho yaliyoko kwenye filamu za microform unajumuisha kiasi cha magazeti themanini ya sasa na ya nyuma ya Afrika Kusini. Machapisho mengine yaliyoko kwenye filamu za microform ni nyaraka za mashirika ya the South African Institute of Race Relations, the Trade Union Congress of South Africa, machapisho katika lugha ya Kitswana, nyaraka kuhusu kifo cha Steve Biko na kuhusu kesi za kisiasa za Afrika Kusini.

Afrika Mashariki na Kati

Mkusanyiko wa magazeti ya Afrika Mashariki na Kati ni mkubwa sana mahsusi kwa nchi za Djibouti, Kenya, Somalia, Tanzania, Congo DRC na Zimbabwe. Mradi wa CAMP unao mkusanyiko uliokamilika wa nyaraka kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wanawake iliyotolewa na the African Training and Research Centre for Women iliyoko katika United Nations Economic Commission for Africa (Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi wa Afrika), Addis Ababa, Ethiopia. Idadi ya machapisho kuhusu Congo DRC na historia yake inazidi vichwa vya habari 250.

Jinsi ya Kujiunga na CAMP

Uanachama wa CAMP uko wazi kwa taasisi au shirika lisilo la kibiashara lenye maktaba na ambalo maslahi yake yanaendeana na yale ya Mradi wa CAMP.

Taasisi wanachama wana haki ya kuazima machapisho kupitia mpango wa maktaba wa kuazimana machapisho au kwa kipepesi au kutuma kwa njia ya pepe. Yote haya hugharamiwa na CAMP kufuatana na taratibu za CRL za kuazimisha machapisho. Haya machapisho yanapatikana kupitia orodha ya kwenye tovuti ya Center for Research Libraries, katika ukurasa wake wa mwanzo: http://www.crl.edu; pia yanapatikana kupitia OCLC.  

Vilevile, wanachama hununua machapisho katika filamu za microform yaliyotolewa na mradi kwa kuzingatia vizuizi husika vya hati miliki.

Wanachama pia hushiriki katika mpango wa uelekezaji na uendeshaji wa mradi. Katika mpango huo, wanachama hupendekeza na kupiga kura kuhusu uagizaji wa machapisho au kuyatolea filamu za microform chini ya mradi.

Uanachama unatathminiwa kila mwaka (kuanzia mwezi wa saba). Wanachama kamili waliopo Amerika Kaskazini wanatozwa ada ya uanachama ya $800 kwa mwaka (zile taasisi ambazo si washirika wa CRL wanatozwa $1300). Mpangilio wa uanachama wa kimataifa wapatikana pia. 

Angalia masharti ya mradi kwa maelezo zaidi.

Fomu ya kuomba uanachama inapatikana katika tovuti: http://www.crl.edu/area-studies/camp
 
Kwa maelezo zaidi kuhusu uanachama wa CAMP, wasiliana na:
Project Coordinator, CRL/GRN
Center for Research Libraries
6050 South Kenwood Avenue
Chicago, IL 60637-2804
USA
Simu: 1-773-955-4545

Habari Kuhusu Machapisho ya CAMP na Upatikanaji Wake

Machapisho yote yaliyopatikana kupitia mradi wa CAMP huifadhiwa CRL. Hadi leo, CAMP imenunua au kutoa katika filamu za microform zaidi ya vichwa vya habari 8,000. Katika hayo, 7,590 yalipatikana na kuorodheshwa kabla ya mwaka 1985 na yamejumuishwa kwenye orodha kama CAMP Catalog: Cumulative Edition (Chicago: Center for Research Libraries. 642 p.).  Yale machapisho yaliyopatikana baada ya mwaka 1985, pamoja na yale ambayo orodha yake imetolewa kwa njia ya chapa, yako katika mtandao wa CRL kama orodha ya kuhifadhi takwimu.

Pamoja na orodha ya seti za filamu za microform, kuna fahirisi zilizochapwa kuonyesha yaliyomo kwenye hizo seti, na miongozo ya vibiringo vyake.

Machapisho mapya yanayoagizwa na CAMP huorodheshwa katika jarida la CRL litolewalo kila baada ya miezi miwili, Focus on the Center for Research Libraries, na katika kumbukumbu za CAMP, Africana Libraries Newsletter, zinazochapwa kila baada ya miezi minne. 

Machapisho yote hupatikana kupitia mpango wa maktaba wa kuazimana machapisho kwa wanachama wa CAMP. Upatikanaji wa haya machapisho kwa taasisi ambazo si wanachama wa CAMP au CRL, hufuatana taratibu za matumizi ya haya machapisho kwa wasio wanachama. Mradi wa CAMP hutengeneza nakala za haya machapisho na kuziuza kwa sababu huhifadhi nakala halisi za filamu hizi za microform.

The Center for Research Libraries

ambayo iliundwa mwaka 1949, ni taasisi ya ushirikiano inayoendeshwa na taasisi wanachama zaidi ya 240 ambao ni vyuo vikuu, vyuo na maktaba za utafiti. The Center for Research Libraries hukusanya, huhifadhi, hutoa orodha kurahisisha upatikanaji, na huazimisha mkusanyiko wake wa zaidi ya machapisho milioni 5.

CAMP Preserves Kenyan Newspaper Taifa Leo

CAMP Preserves Kenyan Newspaper Taifa Leo

CAMP has microfilmed issues of Taifa Leo from November 2004 to May 2010. Taifa Leo is the only Kiswahili daily paper published in Kenya.

CAMP Preserves Government Documents from the Plateau State of Nigeria

Documents from the 1970s through the 2000s include annual reports of state agencies, state budgets, government white papers on issues of the day, texts of speeches, and other ephemeral material.